top of page

Miradi yetu nchini Kolombia inalenga kulinda hekari milioni 1.2 ya misitu iliyo katika hatarini katika idara za Vaupés, Putumayo na Chocó. Tukiwa tunalenga uwazi na michakato jumuishi, tunashirikiana na jamii za wenyeji na Wakolombia wenye asili ya Afrika kuboresha ustawi wa maelfu ya familia na kutunza viumbe hai vilivyo kwa wingi katika eneo hilo.

Tuna miradi 5 inayoendelea ndani ya mojawapo ya nchi zenye viumbe hai wengi zaidi duniani, Kolombia. Miradi hiyo inapatikana katika maeneo mawili tofauti kimazingira: Amazon na Pwani ya Pasifiki.

MATUNZIO YA PICHA

>50k

JAMII
WASHIRIKA

520,000

HEKARI
ZA MISITU ZILIZOLINDWA

37

SPISHI ZILIZO HATARINI
ZILILINDWA

809,000

YA UCHAFUZI WA tCO2e
ILIZUIWA KWA MWAKA

_MG_2335.jpg

ENEO LA KIMAZINGIRA LA PASIFIKI LA KOLOMBIA

logo

WASHIRIKA

WA JAMII

Miradi yetu 3 katika idara ya kipwani ya Chocó ni nyumbani kwa zaidi ya wanajamii 50,000, wengi wao wakiwa Wanakolombia wenye asili ya Afrika.

Himaya za jamii za Wakombia wenye asili ya Afrika zipo zaidi katika maeneo ya mashambani, ambayo pia ni baadhi ya maeneo yenye ukwasi wa rasimali katika nchi hiyo. Hali hii imesababisha miongo mingi ya dhuluma na vurugu kutokana na kupatikana katika njia panda ya mgogoro mkali kati ya makundi yaliyojiami.

Jamii za Wakolombia wenye asili ya Afrika zimejipanga kwenye mabaraza thabiti na yaliyo katika nchi pana na yanayotambuliwa (Consejos comunitarios de comuidades negras) ambayo wanatumia kutawaka na kuweka ubabe wao wa kihimaya na matamanio binafsi.

Jamii za ndani zilizo katika maeneo ya mradi zimejipanga na zinawakilishwa na mabaraza 11 ya jamii. Mabaraza haya ni muhimu katika kuamua jinsi ya kutumia mapato yanayotokana na mradi ambapo wamechuma kwa kulinda misitu yao, ambayo ni muhimu katika kuweka mustakabali stahimilivu yenye matamanio binafsi.

MAKALA YA 01

LA NEGRA TAMBORENA

Msikilize Yajaira Salazar, mshairi Mkolombia mwenye asili ya Afrika anayeishi katika mradi wa Bajo Atrato

Sikiliza

MAKALA YA 02

UKAME CHOCÓ

Sikiliza jamii zinapozungumza kuhusu jinsi msimu wa ukavu ulivyoathiri maisha yao ya kila siku na mbinu mbadala na endelevu zinazoweza kutekelezwa ili kuboresha hali zao

Sikiliza

MASIMULIZI YA JAMII

MIKUTANO YA FPIC
Pata maelezo zaidi

Mikutano ya kupata Idhini Huru, Ya Mapema Iliyofahamishwa ni muhimu katika miradi yetu (FPIC)   Jamii zina haki ya kuamua vipaumbele vyako binafsi kulingana na imani zao, asasi na/au himaya au matumizi yao binafsi.

HISTORIA USHIRIKIANO
Pata maelezo zaidi

Tulianza kazi yetu nchini Kolombia mwaka 2018 kama ushauri wa kiufundi kwa mpango wa Páramos na Bosques uliofadhiliwa na USAID

UBADILISHANAJI WA MAARIFA
Pata maelezo zaidi

Tunalenga kukuza uwezo ndani ya jamii za ndani na kubadilishana maarifa ya kisanyansi na kizazi ili kukuza maamuzi yanayofaa maeneo mahususi ambayo yana ufanisi katika kuhifadhi misitu.

MUHIMU
SPISHI ZA WANYAMA PORI

° Saguinus oedipus 

TAMARINI MWENYE KICHWA CHEUPE

Tamarini ambaye ni mnyama mdogo mwenye uzani ulio chini ya pauni, ambaye amepewa jina lake kutokana na nywele nyeupe iliyo kichwani pake. Tamarini ni miongoni mwa wanyama walio hatarini kutoweka duniani, kukiwa na takriban 6,000 pekee waliobaki msituni. Spishi hii inapatikana sana kaskazini magharibi mwa Kolombia, na makazi yao ya misitu ya tropiki yanaharibiwa kwa minajili ya ufugaji wa mifugo, kilimo na maendeleo ya miji. Wanyama hawa pia hunaswa na kuuzwa kwa njia haramu kama wanyama vipendwa.

° Panthera Onca 

JAGUA

Jagua ni mnyama mkubwa zaidi wa jamii ya paka kutoka Amerika Kusini na wana umuhimu mkubwa wa kiekolojia, kitamaduni na kiroho. Inakadiriwa kuwa takriban jagua 15,000 ndio wamesalia nchini Kolombia na takriban Jagua 170,000 wapo katika bara zima la Amerika. Spishi hii ambapo wakati mmoja ilipatikana kuanzia kusini wa Marekani hadi kaskazini mwa Ajentina, lakini upatikanaji wake umekatwa hadi nusu na spishi hii inapotea katika nchi kadhaa, kutokana na matishio ya kimsingi ya kupoteza makazi, biashara haramu na mabadiliko ya tabianchi.

° Ara ambiguus 

KASUKU WA KIJANI

Akiwa na rangi angavu za kijani, Kasuku wa Kijani huenda asikanganye na ndege yeyote mwingine. Kasuku wa Kijani ndiye kasuku wa tatu kwa uzito duniani na anaweza kuisha kwa hadi miaka 70. Ndege anayependa kutangamana, Kasuku wa Kijani huishi katika makundi ya familia ya ndege watano au sita, ambayo hutembelea miji ya karibu ikitafuta miti yenye matunda ambayo awanaweza kula. Kutokana na kupotea kwa makao na biashara haramu ya wanyama vipendwa, spishi hii inazingatiwa kuwa Hatarini Zaidi kulingana na IUCN.

° Tapirus bairdii 

BAIRD'S TAPIR

Baird's tapir ni mnyama mkubwa mlaji nyasi mwenye umbo kama la nguruwe na pua refu. Baird's tapir wana nafasi muhimu katika mazingira yao kwa kutawanya mbegu, kushikilia mahusiano ya kutegemeana na ndege wapenda usafi (kama vile karakara mwenye kichwa cha manjano) na kutoa chanzo muhimu cha lishe kwa wanyama wala nyama kama vile jagua. Kutokana na matishio ya kugawanywa kwa makao na kupoteza makao, spishi hii inazingatiwa kuwa Ipo Hatarini kulingana na IUCN.

​MISITU

​​Miradi yetu 3 katika Chocó inafanyika katika zaidi ya hekari  500,00 za msitu

Misitu ya tropiki ya Chocó-Darién katika pwani ya Pasifiki ya Kolombia inaunda mojawapo ya maeneo makuu kumi bora ya viumbe anuwai vya dunia. Maeneo ya mradi yana ukwasi wa spishi za kipekee (spishi ambazo hazipatikani kwingineko kwenye sayari hii) na aina mbalimbali za mazingira yenye thamani kama vile matumbawe, vinamasi, misitu yenye mafuriko, misitu mikavu na misitu ya mawingu. Matishio kwa misitu yanatokana na upanuzi bila kupangwa wa sekta ya kilimo, kulima mazao haramu na uvunaji wa mbao kwa njia haramu. Ili kusaidia kupunguza sababu za ukataji miti, shughuli za mradi wetu zinajumuisha ongezeko la ufuatiliaji na ulinzi wa vibadala vya kiuchumi vinavyotegemea jamii, kilimo cha uhifadhi na kuunda nafasi za ajira.

MAI NDOMBE

DRC

Katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), mradi wa REDD+ wa Mai Ndombe hulinda hekari 300,000 za msitu.

Pata maelezo zaidi

ENEO LA KIMAZINGIRA LA AMAZON KOLOMBIA

Katika Eneo la Kimazingira la Kolombia, tuna miradi 3 tunayounda ya kulinda hekari 750,000 ya misitu. 

Pata maelezo zaidi

GUNDUA MIRADI YETU MINGINE

ASILI

Zaidi ya nusu ya eneo la bara la Kolombia ina misitu asili, lakini katika miaka sita iliyopita, nchi hiyo imepoteza karibu ekari milioni 1 ya misitu, ambayo ni sana wa na takriban viwanja milioni 1 vya kandanda. Hali hii imesababisha mgogoro wa mara kwa mara wa kijamii na mazingira ambao umeathiri wanajamii za misitu, tabianchi za eneo na viumbe hai vya nchi hiyo.

Ukataji wa miti nchini Kolombia umesababisha hali changamano ya vigezo vya kihistoria na kijamii na kiuchumi, lakini kimsingi unahusishwa na upanuzi wa haraka wa shughuli za kilimo. Hii inajumuisha unyakuzi wa ardhi kwa ajili ya ufugaji wa mifugo na shughuli haramu, kama vile uvunaji na matumizi mabaya ya madini yenye thamani, mimea haramu kama vile majani ya coca na mbao za kibiashara.

Baadhi ya sababu kuu za kuongezeka kwa ukataji wa miti ni ukosefu wa njia mbadala za uzalishaji na endelevu za kiuchumi kwa jamii za ndani, mifumo dhaifu ya kikanda na utawala wa ndani, serikali kukosha kujihusisha vya kutosha na vita vinavyoendelea vinavyohusisha silaha.

USEFUL LINKS

MIRADI

Wildlife Works ilianza kazi nchini Kolombia mwaka wa 2018 ili kutoa usaidizi wa kiufundi katika awamu zote za utekelezaji wa miradi 8 ya REDD+ iliyofadhiliwa na USAID katika pwani ya pasifiki ya Kolombia, almaarufu Portafolio REDD+ Pacífico or Portafolio BioREDD. Muda mfupi baadaye, tulianzisha mchakato wetu binafsi wa kutafuta vyanzo na maendeleo ya mradi nchini Kolombia.

Miradi katika Eneo la Kiuchumi la Pwani ya Pasifiki (Chocó) ni pamoja na:

bottom of page