top of page

Miradi yetu nchini Kolombia inalenga kulinda hekari milioni 1.2 ya misitu iliyo katika hatarini katika idara za Vaupés, Putumayo na Chocó. Tukiwa tunalenga uwazi na michakato jumuishi, tunashirikiana na jamii za wenyeji na Wakolombia wenye asili ya Afrika kuboresha ustawi wa maelfu ya familia na kutunza viumbe hai vilivyo kwa wingi katika eneo hilo.

 Tuna miradi 5 inayoendelea ndani ya mojawapo ya nchi zenye viumbe hai wengi zaidi duniani, Kolombia. Miradi hiyo inapatikana katika maeneo mawili tofauti kimazingira: Amazon na Pwani ya Pasifiki.

MATUNZIO YA PICHA

2,900

JAMII
WASHIRIKA

540,000

HEKARI
ZA MISITU ZILIZOLINDWA

2

SPISHI ZILIZO HATARINI

ZILILINDWA

740,000

YA UCHAFUZI WA tCO2e
ILIZUIWA KWA MWAKA

DJI_0024.jpg

ENEO LA KIMAZINGIRA LA KOLOMBIA

logo

WASHIRIKA

WA JAMII

Miradi yetu 2 katika eneo la kimazingira la Amazon ya Vaupés na Putumayo ni nyumbani kwa wanajamii 2,000, wengi wao wakiwa ni Wenyeji wa eneo hilo.

Katika misitu ya Amazon ya Kolombia, Wenyeji wamekuwa katika mstari wa mbele kulinda ardhi na rasilimali zao kwa maelfu ya miaka. Umuhimu wa kiroho na uhusiano wa dhati na misitu umesaidia kudumisha afya na ukwasi wa viumbe anuwai katika mazingira haya yenye thamani kubwa.

 

Katika Vaupes, Muungano wa Mamlaka za Jadi za Wenyeji wa Yapú Zone (ASATRIZY) unajumuisha jamii 8 na makundi ya Wenyeji ya Carapana, Tatuyo, Tucano, Bara na Tuyuca. Muungano wa Mamlaka za Jadi za Wenyeji wa Querarí (ASATIQ) unajumuisha jamii 17 na kundi la Wenyeji la Cubeo.

Katika miradi hii, vizazi vya maarifa ya jazi vinafumwa pamoja kwa kupewa mbinu za kisasa za kusaidia kuongeza utoshelevu wa chakula idadi ya watu inapozidi kukua, kupungua kwa hali ya kutegemea mbinu zisizoendelevu za "kukata na kuchoma" mashamba, kutambua nyenzo mbadala za ujenzi na kuunda nafasi za kazi za vyanzo mbadala vya kuchuma mapato.  Mabaraza ya Jamii yaliyoundwa kindani hujitawala kwa mujibu wa kaida na desturi za kila jamii binafsi na huendelea kuelekeza mkono wa matumizi ya mapato yanayotokana na mradi.

MAKALA YA 01

KUTENGENEZA MUUNGANO

Diego Ramírez kutoka katika Muungano wa Mamlaka za Wenyeji wa Yapú (ASATRIZY) anasema sababu zake za kwa nini alichagua Wildlife Works kama rafiki.

Soma zaidi

MAKALA YA 02

MUJERES MÚRUI

Kutana na Victoria Yaci, kiongozi wa kike anayeongoza harakati za kuwezeshwa kwa wanawake katika jamii yake, Puerto Refugio.

Soma zaidi

MASIMULIZI YA JAMII

MIKUTANO YA FPIC

Pata maelezo zaidi

Tunawajipatia wajibu wa kupata idhini ya kina na inayofaa kitamaduni ambayo ni ya huru, ya mapema na iliyofahamishwa (FPIC). Hii inamaanisha kubuni utamaduni na kuweka vipindi mahususi vya mafunzo kuhusu soko la hewakaa ili kuhakikisha kuwa wanafanya uamuzi uliofahamishwa, hususan ikiwa jamii ina desturi semwa. Tunaweka taratibu wazi za kushughulikia malalamishi na jamii zinafahamu kuwa zina haki ya kuondoa idhini yao katika kipindi kizima cha mradi.

​-GILDARDO CALDERÓN
PUTUMAYO, COLOMBIA

"Tunategemea Dunia Mama yetu ili kupata bidhaa tunazohitaji kwa ajili ya familia zetu. Hiyo ndiyo sababu ni jukumu letu kudumisha afya ya himaya zetu."

MAWASILIANO YA WAZI
Pata maelezo zaidi

Mojawapo ya vigezo vya ufanisi wa kazi ya timu ni mawasiliano bayana na ya wazi.
Pamoja na wanajamii, tumwebuni na kuweka misururu ya bodi zilizo na taarifa zote kuhusu mikutano, michakato ya mradi na namba za mawasiliano ili watu wote wanaoishi katika himaya hizo wanajumuishwa kwenye miradi na wanaweza kuhusika katika shughuli tofauti za mradi.

UTAWALA WA JAMII
Pata maelezo zaidi

Katika kila mradi ulioundwa na Wildlife Works, jamii huchagua watu walio katika jamii mbalimbali walio ndani ya himaya na ambao ni sehemu ya mradi wa uhifadhi unaonuiwa kuendelezwa. Kamati hii inajukumu la kuhakikisha masilahi ya kila jamii, kupendekeza uwekezaji wa mapema na kufuatilia mchakato mzima.

KAZI ZA KULINDA VIUMBE ANUWAI
Pata maelezo zaidi

Walinzi wa mazingira ambao ni Wenjeji walioajiriwa vijijini husaidia kufuatilia na kulinda Wanyama pori ndani ya eneo la mradi.

MUHIMU
SPISHI ZA WANYAMA PORI

° Boa constrictor 

CHATU

Chatu ni maarufu kama mojawapo ya nyoka kubwa zaidi kwenye sayari yetu. Kwa jumla, chatu mmoja ni kati ya mita 2 na 3 kwa urefu, wa kike wakiwa wakubwa kuliko wa kiume. Chatu hupata hisia kuhusu mazingira yao kupitia mitetemo, mawimbi ya mwangaza, kwenye mwake wa ultravioleti na ishara za kemikali ambazo wanapata kupitia ndimi zao. Tofauti na nyoka wenye sumu, chagu huwafunga windo zao kwenye miili yao na kukunjama hadi windo afe kutokana na kukosa kupumua. Chatu wana nafasi kubwa ya kiekolojia kama walaji wa ndege na wanyama wadogo. Ni walaji muhimu wa aina za panya, ambao bila chatu kuwema wanaweza kuwa waharibifu katika baadhi ya maeneo na kubeba magonjwa yanayoathiri binadamu. Kukusanywa kupita kiasi kwa ajili ya biashara ya wanyama vipendwa na kuuawa moja wa moja kumekuwa na athari hasi kwa idadi kubwa ya Chatu.

° Panthera Onca

JAGUA

Jagua ni mnyama mkubwa zaidi wa jamii ya paka kutoka Amerika Kusini na wana umuhimu mkubwa wa kiekolojia, kitamaduni na kiroho. Inakadiriwa kuwa takriban jagua 15,000 ndio wamesalia nchini Kolombia na takriban Jagua 170,000 wapo katika bara zima la Amerika. Spishi hii ambapo wakati mmoja ilipatikana kuanzia kusini wa Marekani hadi kaskazini mwa Ajentina, lakini upatikanaji wake umekatwa hadi nusu na spishi hii inapotea katika nchi kadhaa, kutokana na matishio ya kimsingi ya kupoteza makazi, biashara haramu na mabadiliko ya tabianchi.

 °Inia geoffrensis

POMBOO WA MTO AMAZON

Pomboo wa mto Amazon, almaarufu kama pomboo wa mto wa pinki, ni viumbe wa kuvutia wanaopatikana katika mifumo ya maji safi katika nchi sita za Amerika Kusini. Pomboo hawa hukabiliana na maji ya mto Amazon kimsingi kwa kufuata mwangwi, na wana nafasi muhimu katika kuleta usawa kwenye makazi, wakiwa wanyama wakubwa wanaosaidia kudhibiti idadi ya samaki na kudumisha mazingira salama. Rangi yao ya kipekee ya pinki inadhaniwa kuwa inatokana na mishipa ya damu iliyo karibu na sehemu ya ngozi ambayo inaweza kujitokeza zaidi wakiwa wachangamfu, sawa na jinsi binadamu huona haya. Hata hivyo, sababu halisi ya rangi yao ya pinki inasalia kuwa mada inayochunguzwa kisanyansi. Licha ya umuhimu na upekee wao, pomboo wa mto Amazon wanakabiliwa na matishio kama vile uharibifu wa makazi, uchafuzi na kunaswa katika shughuli za uvuvi bila kukusudiwa. Vigezo hivi vimesababisha kupungua kwa idadi yao, na kufanya waorodheshwe kama wanyama walio hatarini na IUCN.

 ° Ramphastos tucanus

TOKANI WENYE SHINGO NYEUPE

Tokani wenye shingo nyeupe huishi kiasilia kote kwenye Amazon kusini mashariki mwa Kolombia. Tokani wenye shingo nyeupe ni ndege wa kustaajabisha wenyeji wa misitu ya tropiki ya Amerika ya Kati na Kusini. Tokani hawa wanatambulika kwa urahisi kupitia mkusanyiko wa manyoya yao, mwili mweusi, kifua cha rangi ya manjano angavu na madoa meupe ya kipekee kwenye shingo lake. Sifa yao ya kipekee zaidi ni mdomo wao mkubwa wenye rangi, ambao unatumika kufanya mambo kadhaa, ikiwa ni pamoja kufikia matunda, kunasa wadudu na kuimba. Tukani wenye shingo nyeupe huishi mitini na hutumia muda wao mwingi katika misitu, ambapo wanakaa katika makundi madogo au jozi. Ni walaji wa matunda, matunda yakiwa ni mlo wao mkuu, lakini pia wanakula wadudu na reptila wadogo. Ingawa idadi yao inazingatiwa kuwa thabiti, ukataji wa miti na kupoteza makao ni hali zinazotishia maisha yao, kwa kuwa wanategemea mazingira thabiti ya misitu. Juhudi za kulinda mazingira yao na kutoa uhamasisho kuhusu uhifadhi wao ni muhimu ili kuhakikisha kuwa ndege hawa wenye bashasha wanaendelea kuwepo kwenye makao yao asili.

​MISITU

Kolombia ni nyumbani kwa asilimia 10 ya misitu mipana ya Amazon, mapafu ya dunia yetu.

Misitu ya Putumayo na Vaupés ina msitu isiyogawanywa na yenye unyevunyevu ya tropiki. Spishi nyingi za thamani, kama vile rosewood na mkangazi, zinaweka msitu huo katika hatari kutokana shughuli haramu za utafutaji mbao. Isitoshe, uvunaji haramu wa mchanga mweusi na madini ya thamani ya chuma yanaweka eneo hilo hatarini. Shughuli za mradi za kusaidia kupunguza sababu hizi za ukataji wa miti ni pamoja na ongezeko la ufuatiliaji na ulinzi, kilimo cha hifadhi na uundaji wa nafasi za kazi.

KASIGAU CORRIDOR

KENYA

Nchini Kenya, mradi wa REDD+ wa Kasigau Corridor hulinda hekari 200,000 za msitu.

Pata maelezo zaidi

ENEO LA KIMAZINGIRA LA PASIFIKIKOLOMBIA

Katika Eneo la Kimazingira la Pasifiki la Kolombia, tuna miradi 3 tunayounda ya kulinda hekari 500,000 ya misitu.


Pata maelezo zaidi

GUNDUA MIRADI YETU MINGINE

ASILI

Zaidi ya nusu ya eneo la bara la Kolombia ina misitu asili, lakini katika miaka sita iliyopita, nchi hiyo imepoteza karibu ekari milioni 1 ya misitu, ambayo ni sana wa na takriban viwanja milioni 1 vya kandanda. Hali hii imesababisha mgogoro wa mara kwa mara wa kijamii na mazingira ambao umeathiri wanajamii za misitu, tabianchi za eneo na viumbe hai vya nchi hiyo.

Ukataji wa miti nchini Kolombia umesababisha hali changamano ya vigezo vya kihistoria na kijamii na kiuchumi, lakini kimsingi unahusishwa na upanuzi wa haraka wa shughuli za kilimo.
Hii inajumuisha unyakuzi wa ardhi kwa ajili ya ufugaji wa mifugo na shughuli haramu, kama vile uvunaji na matumizi mabaya ya madini yenye thamani, mimea haramu kama vile majani ya coca na mbao za kibiashara.

Baadhi ya sababu kuu za kuongezeka kwa ukataji wa miti ni ukosefu wa njia mbadala za uzalishaji na endelevu za kiuchumi kwa jamii za ndani, mifumo dhaifu ya kikanda na utawala wa ndani, serikali kukosha kujihusisha vya kutosha na vita vinavyoendelea vinavyohusisha silaha.

MIRADI

Wildlife Works ilianza kazi nchini Kolombia mwaka wa 2018 ili kutoa usaidizi wa kiufundi katika awamu zote za utekelezaji wa miradi 8 ya REDD+ iliyofadhiliwa na USAID katika pwani ya pasifiki ya Kolombia, almaarufu Portafolio REDD+ Pacífico or Portafolio BioREDD. Muda mfupi baadaye, tulianzisha mchakato wetu binafsi wa kutafuta vyanzo na maendeleo ya mradi nchini Kolombia.

Miradi katika Eneo la Kimazingira la Amazon (Putumayo na Vaupes) ni pamoja na:

USEFUL LINKS

bottom of page