top of page
220505 Filip Agoo - Everland - Southern Cardemon Cambodia C1_00189.jpg

KWA SERIKALI

logo

Soko la Kujitolea la Hewakaa ni fursa

ya kimkakati kwa serikali mwenyeji:

kufikia fedha za tabianchi kwa masharti yao binafsi

kufanya kazi na sekta ya kibinafsi kama washirika sawa, si wafadhili

kutumia uhifadhi wa misitu kufadhili maendeleo ya matamanio binafsi huku zikichangia katika tabianchi ya dunia na malengo ya uendelevu

kufadhili maendeleo ya kitaifa na mitaani katika kiwango ambacho ni cha mageuzi na chenye athari za vizazi

Kwa nini ushirikiane nasi?

Wildlife Works inaongoza katika kuunda miradi iliyoanishwa ya REDD+ ambayo inahakikisha kuwa nchi wenyeji zinaweza kutumia mbibu za ufadhili kukidhi malengo yao ya sera, tabianchi, uhifadhi na maendeleo.

Tuna uzoefu wa miaka 25 hali ambayo imetufanya tuwe mshirika wa kuaminiwa na jumuiya za misitu na serikali.

Kama wataalamu wanaotambuliwa kote duniani katika REDD+, sisi ni washauri wanaoaminiwa na serikali ambazo vingependa kufuata mfumo wa kitaifa wa REDD+ unaoanisha miradi kwenye mpango wa kimaeneo.

Tuliwezesha utiaji sahihi wa ERPA kati ya Hazina ya Hewakaa ya Benki ya Dunia FCPF na Serikali ya DRC, na kufanya Mpango wa Ndombe ER kuwa mpango wa kwanza duniani kufaulu katika kuoanisha mradi ndani ya mpango wa kimaeneo.

KAMPUNI INAYOENDESHWA NA MAADILI

Mfumo wetu wa ugavi wa mapato unalenga kuwezesha malengo ya nchi wenyeji ili kutoa maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa jamii za ndani kupitia makubaliano ya ugavi wa mapato kwa usawa, huku tukifadhili matamanio ya nchi wenyeji kuingia katika mpwito wa kawi safi.

docoratice vector image
docoratice vector image

MCHAKATO NYUMBUFU ULIOFAFANULIWA VYEMA

Tuna mchakato ambao umejaribiwa na wa kweli wa maendeleo na utekekelezaji wa mradi unaotuwezesha kufanya mambo kulingana na mahitaji na utamaduni wa kila eneo huku pia ukifanya kazi kwa ufanisi kuanza kuzalisha mapato kutokana na mradi kwa ajili ya washirika wetu wa ndani ya nchi.

docoratice vector image

MAUZO NA UFADHILI THABITI

Tuna mkakati wa kipekee na wa moja kwa moja wa mauzo kupitia kampuni yetu ya kipekee ya mauzo, Everland Marketing ambao hutambua na kujenga mahusiano ya muda mrefu na wateja na wawekezaji wa kishirika walio na ari kuhusiana na tabianchi. Tumeweka ufadhili kupitia washirika wetu Hartree Partners ili kukuza awamu mpya ya miradi 20 kote duniani ambayo itapunguza uchafuzi kwa tani milioni 20 za CO₂e kila mwaka na kutoa ufadhili wa dola za Marekani bilioni $2.

docoratice vector image

MISINGI MIPANA NA YA UFANISI

Tuliunda njia mpya kabisa ya ugavi wa msingi ambayo inasambaza Viwango vya kitaifa vya Uchafuzi wa vya Marejeleo ya Misitu (FREL) kulingana na hatari ya ukataji wa miti siku zijazo. Njia ya kuoanisha miradi kwenye mipango ya kimaeneo hukakikisha kuwa serikali za kitaifa zinaweza kutumia kwa ufanisi Soko la Kujitolea la Hewakaa ili kuweka pamoja ufadhili wa kifedha katika maeneo ya misitu yenye hatari kubwa zaidi huku zikichangia Michango Iliyobainishwa Kitaifa.

Soma zaidi kuhusu mbinu yake katika Mfumo wetu wa Desturi Njema nchini DRC.

Mask group (1).jpg

Wasiliana nasi ikiwa wewe ni sehemu ya serikali ya kitaifa inayopania kutekeleza REDD+ ili kufanikisha malengo yako ya uhifadhi na maendeleo.

bottom of page