top of page
Filip-C-Agoo-Everland-Marketing-Congo-3266-WEB-low-resolution.jpg

KWA SEKTA YA KIBINAFSI

Wildlife Works Logo

Ni masilahi ya kila biashara kuwekeza katika afya ya sayari kupitia malipo ya hewakaa yanayotegemea asili. Utafiti kutoka World Economic Forum unaonyesha kuwa angalau asilimia 50 ya GDP ya dunia inategemea asili, na kwamba mabadiliko ya tabianchi yatayumbisha pakubwa biashara ya kimataifa.  Hata hivyo, uwekezaji katika kulinda asili bado haujafika mahali unapofaa, hususan katika maeneo ambayo yameathiriwa zaidi na mabadiliko ya tabianchi.

Tunahitaji suluhu zote ili kukabiliana na janga la tabianchi, na ukubwa na ushawishi wa soko kwa sasa bado ni kani kubwa zaidi kusogeza hatua ya tabianchi. Mabadiliko ya sera, teknolojia na matumizi yanayopaswa kuondoa hewakaa kwenye uchumi wetu hayafanyiki haraka inavyotakiwa ili kukomesha mabadiliko ya tabianchi. Hatua ya tabianchi katika sekta ya kibinafsi inapaswa kuwa ya kijasiri zaidi sasa kuliko awali.

Miradi ya REDD+ iliyo kwenye Soko ya Kujitolea ya Hewakaa (VCM) kwa sasa ndiyo zana ya ufanisi zaidi iliyo karibu inayoweza kutumika kwa kiwango kikubwa kulinda misitu kwenye sayari yetu na kufikia malengo yetu ya mabadiliko ya tabianchi.  Kama ambavyo ripiti ya hivi punde ya Jopo la Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi la Umoja wa Mataifa (IPCC) inavyosema, kudumisha mazingira asili ni mojawapo ya chaguo muhimu zaidi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Miradi ya uhifadhi itapanuka tu na kufanikisha katika kiwango kikubwa kinachohitajika ili kukomesha ukataji wa miti kwa ufanisi ikiwa sekta ya kibinafsi itawajibika na kuwekeza katika mbinu za soko kama vile REDD+. Kuwekeza katika jumuiya za misitu, ambazo zinalinda mazingira makubwa ya viumbe anuwai kwenye sayari yetu, ni njia muhimu ya kuchukua hatua dhidi ya tabianchi sasa.


Wale wanaopinga malipo ya mauzo ya hewakaa kimsingi wanafanya hivyo kwa sababu hawana ufahamu kuhusu athari chanya za kimageuzi ambazo miradi ya ubora wa juu na zinazolenga jamii za hewakaa ya misitu hufanya.  Mapingamizi haya yanapuuza mitazamo ya jumuiya za misitu katika Nchi za Kusini za Dunia ambazo huendeleza miradi inayotegemea haki ya REDD+.

Utafiti unaonyesha kwamba kampuni zinazoshiriki katika ununuzi wa hewakaa ndizo ambazo hufanya juhudi kubwa la kupunguza uchafuzi wao, na kufanya juhudi maradufu za kuondoa hewakaa ikilinganishwa zile ambazo hazifanyi hivyo.

 

Tunaendelea kuhimiza wanunuzi kuwajibikia na kuripoti uchafuzi wao, athari zao kwenye kupoteza viumbe anuwai, na kutumia malipo ya mauzo ya hewakaa ya ubora wa juu kama zana muhimu ya kulinda misitu kwa ajili ya malengo yetu ya kupunguza athari za tabianchi duniani.

Miradi ya Wildlife Works imeleta athari isiyopimika na inayoweza kuthibitishwa kwa:

JAMII

Uwekezaji wa miradi yetu kwenye mipango ya maendeleo ya washirika wetu wa kijamii tayari umeleta athari kubwa za kivizazi. Kwa mfano, walionufaika na mpango wa ufadhili wa masomo ya wanafunzi katika mradi wetu wa Kasigau Corridor REDD+ wanarejea kutoka kwenye vyuo vikuu kama walimu na viongozi katika jamii.

Community members in Cambodia
decoratice vector image
Elephant in Kenya
decoratice vector image

VIUMBE ANUWAI

Miradi ya Kasigau Corridor na Mai Ndombe REDD+ imeshuhudia kurejea kwa spishi muhimu za wanyama pori baada ya kuanza kwa mradi.

Forest
decoratice vector image

TABIANCHI YETU

Hekari milioni 1.7 ya misitu iliyokuwa hatari imelindwa, hali iliyozuiwa mamilioni ya tani ya uchafuzi wa hewakaa kutolewa.

Wildlife Works inaongoza katika
REDD+ inayotegemea haki

Wildlife Works inaongoza katika REDD+ inayotegemea haki, ikiwa na uzoefu wa zaidi ya miaka 25 ikishirikiana moja kwa moja na jumuiya za misitu zinazounda suluhu za uhifadhi zinazotegemea soko. Tulikuwa wa kwanza kufanikisha malipo ya kwanza yaliyothibitishwa ya shughuli ya kuzuia ukataji wa mti kupitia REDD+, na miradi yetu imepewa hadhi ya juu kwa sababu ya uwazi, kina cha sayansi, na muhimu zaidi kwa kuheshimu haki za jamii za ndani.

 

Jifunze zaidi kuhusu uongozi wetu wa soko.

Kwa nini unapaswa kuwekeza kwenye suluhu zinazotegemea asili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi?

Mask group.jpg

Jiunge na wateja wetu wa sasa katika

kuweka mustakabali chanya wa asili.

bottom of page