top of page
Filip-C-Agoo-Everland-Marketing-Congo-1901-WEB-low-resolution.jpg

DESTURI NJEMA ZA DRC

logo

Inapotekelezwa kwa viwango vya juu zaidi, REDD+ (Kupunguza Uchafuzi kutokana na Ukataji wa Miti na Uharibifu wa misitu) miradi inaweza kusaidia nchi kufanikisha malengo yao ya tabianchi kwa kuleta athari chanya kwa jamii na viumbe anuwai. Kulinda mandhari yenye hewakaa kwa njia endelevu kunahitaji shughuli ya uhifadhi kutumia mbinu inayotegemea haki ambayo inazipa kipaumbele juhudi za Wenyeji na Jamii za Ndani (IPLC) kuhifadhi misitu yao. Manufaa ya miradi ya REDD+ lazima ipatikane nyanjani na watu ambao wanaishi kwenye misitu.

 

Ili kufanikisha lengo hili, Wildlife Works imeshirikiana na Nature Conservancy, ambacho ni kikundi cha watekelezaji bora wa miradi nchini DRC na wanachama wa kundi la kijamii katika kuweka desturi njema za utekelezaji wa miradi ya REDD+ katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

 

Lengo la ripoti hii ni kuwezesha serikali ya DRC, jumuiya za misitu za DRC na wakaguzi wa kimataifa kuweza kutambua kwa ufanisi zaidi hali zinazohitajika ili kufikia utendaji wa kiwango cha juu za REDD+ inayotegemea jamii.

DRC ndiyo inalengwa kwenye ripoti hii, hata hivyo, inaweka msingi bora wa miradi ya REDD+ ya kujifunza kutokana nayo katika nchi mbalimbali zenye ukwasi wa hewakaa zilizo na idadi kubwa ya watu wa IPLC.

Ripoti hii inazungumzia hali changamano za kisheria, kisiasa, kimazingira na kijamii za Wenyeji na Jamii za Ndani (IPLC) nchini DRC, na kutoa maarifa ambayo yanatumika katika kuendesha miradi yenye ufanisi na ubora wa juu ya REDD+ katika maeneo mengine.

 

Inatoa mwongozo, maadili na mapendekezo kwa waundaji wa miradi ya REDD+, na kubainisha misingi ya mradi wowote wa ufanisi wa REDD+.

Hii inajumuisha jinsi ya kutekeleza:

 

  • ​Njia mpya kabisa ya ugavi wa msingi ambayo inasambaza Viwango vya kitaifa vya Uchafuzi wa vya Marejeleo ya Misitu (FREL) kulingana na hatari ya ukataji wa miti siku zijazo. Njia hii hukakikisha kuwa serikali za kitaifa zinaweza kutumia kwa ufanisi Soko la Kujitolea la Hewakaa ili kuweka pamoja ufadhili wa kifedha katika maeneo ya misitu yenye hatari kubwa zaidi huku zikichangia Michango Iliyobainishwa Kitaifa.

  • Utafutaji na ufuatiliaji kwa kina maeneo yaliyozuiwa kukatwa miti kwa ajili ya mradi wowote wa REDD+, kwa malengo yaliyobainishwa wazi, yanayotegemea wenyeji ya kupunguza uchafuzi, na mfumo wa ufadhili ili kuwekeza katika jamii zinazotimiza malengo.

  • Mchakato wa kina na wazi wa Idhini Huru, Ya Mapema Iliyofahamishwa (FPIC) ambayo hukakikisha jamii zinafahamishwa kikamilifu na mapema kabla ya kuanzishwa kwa mradi na zinaheshimiwa kikamilifu kama washirika wa utekelezaji.

  • Mbinu za ufanisi za kushughulikia malalamiko na suluhu kwa IPLC. Hii ni pamoja na kutoa maelezo kuhusu sheria za taifa na desturi njema za kimataifa kuhusu malalamiko na suluhu.

  • Desturi njema za ugavi wa mapato, ambayo imejikita kwenye msingi wa maarifa ambao umedumu kwa miongo miwili ambayo yalitokana na mafunzo kutoka kwenye miradi ya awali, kama vile masharti ya kisheria kutoka kwa serikali na nafasi muhimu ya uwazi na ushirikishaji wa washikadau ili kufanikiwa kukamilisha miradi.

  • Taratibu bora za ufuatiliaji, kuripoti na uthibitishaji wa masuala ya kijamii na viumbe anuwai (MRV), ikiwa ni pamoja na desturi njema za kimataifa za kukadiria na kuonyesha athari ya miradi ya REDD+.

PAKUA PDF YA MB 1.9:
Mfumo wa Utekelezaji wa Desturi Njema za REDD+ za Mradi wa Sekta ya Kibinafsi

Mwongozo huu uliandaliwa na Wildlife Works kwa ushirikiano na kundi la wataalamu bora wa Mradi wa DRC na wanachama wa kikundi cha kijamii cha DRC. Kazi hii ilifadhiliwa na The Nature Conservancy. Umewekwa ili isikiuke kanuni na vigezo vya viwango vinavyoongoza vya kimataifa, huku pia ukiruhusu kutumiwa kwa hali nyumbufu ya soko linalokua kwa kasi la kujitolea la hewakaa na viwango vinavyoendelea kubadilika vinavyotumika.

MFUMO WA DESTURI NJEMA WA UTEKELEZAJI WA MRADI WA REDD+ NCHINI DRC

bottom of page