
MBINU YA WILDLIFE WORKS YA KUPATA IDHINI YA HIARI, YA AWALI NA ILIYO NA TAARIFA YA KUTOSHA (FPIC)
Mfumo wa sasa wa Wildlife Works kwa ajili ya kutekeleza Idhini ya Hiari, ya Awali na Iliyo Na Taarifa ya Kutosha (FPIC) inawakilisha kanuni elekezi tunazojitahidi kudumisha katika kazi yetu. Kutokana na utata wa maendeleo ya mradi katika mazingira mbalimbali, kuanzia hatari za ukataji miti hadi mienendo ya kisiasa na mandhari ya umiliki wa ardhi, tunatumia kanuni hizi kwa busara na kwa uwezo wa kubadilika ili kudumisha usawa katika ushirikiano wetu.
Lengo letu kuu linasalia kuwa thabiti: kujenga ushirikiano wenye mafanikio makubwa unaowezesha uundaji-shirikishi kwa msingi wa kuaminiana, kuelewana na idhini ya pande zote mbili, unaotekelezwa kwa heshima na kwa ufanisi katika maisha yote ya mradi.
MZUNGUKO WA FPIC UNAOENDELEA, USIO NA MTIRIRIKO
Kwa Wildlife Works, FPIC sio tukio la mara moja wala mchakato ulio na mtiririko. Ni mchakato hai inaopumua -mdundo unaobadilika kila wakati wa mazungumzo, uaminifu, na nia ya pamoja. Kama vile ndege aina ya hummingbird anavyopepea, yeye husogea kwa urahisi, hubadilisha mwelekeo kulingana na mihemo ya mahitaji ya jamii, mtiririko wa taarifa na mahusiano yanayoendelea kukua. Inapokubaliwa kama safari inayoendelea badala ya tukio la mara moja, FPIC inakuza ushirikiano wa kina, na kuwaunganisha washikadau katika mfumo wa kufanya maamuzi. Sio idhini tu—ni muungano, uwezo wa mabadiliko, na moyo wa mabadiliko yanayoongozwa kwa kweli na jamii. Soma zaidi kutoka kwa Javier Mancera.
MFUMO WA USHIRIKIANO WA MRADI:
IDHINI ENDELEVU YA JAMII, MAONI NA MAWASILIANO




WEZESHA MICHAKATO NA MAKUBALIANO YA PAMOJA

UTAMBUZI WA WADAU NA MABADILISHANO YA KITAMADUNI
KANUNI
Jenga uhusiano unaoegemea kwenye uaminifu kupitia mabadilishano ya kitamaduni na ya kijamii ili kuelewa na kuheshimu tamaduni, mila na sheria za jamii.
TAMBUA
Tambua wamiliki wote wa ardhi, haki na wamiliki wa matumizi ya kimila na washikadau wengine ambao wataathiriwa na mradi wa uhifadhi.
Tambua matakwa ya kisheria ya kitaifa na miongozo ya ushirikishwaji ya kuzingatia
FAHAMU
Kuza uelewa wa pamoja wa muktadha wa ndani na mapengo ya kitamaduni kupitia mikutano ya kubadilishana kitamaduni ya kabla ya mashauriano
Chora ramani ya ardhi za kimila na wamiliki wa haki za ardhi.
Weka kumbukumbu na uheshimu maarifa ya jadi au ya ndani ndani ya jamii, ikijumuisha mipango iliyopo ya maendeleo.
Heshimu mifumo ya maamuzi ya kimila, upatanishi, na utatuzi wa migogoro iliyopo, pamoja na viongozi au watu wenye ushaawishi wasio rasmi ambao ni muhimu katika kufanya maamuzi ya jamii.
ZIBA MAPENGO
Jenga uelewa wa pamoja kuhusu haki zote, rasilimali, ardhi na maeneo kwa kuzingatia sheria za kimila kupitia uchoraji wa ramani shirikishi.
Ikionekana ni muhimu, jumuisha tathmini ya umiliki wa ardhi au uhakiki wa hali ya ardhi.
Hakikisha ushiriki wa maana wa wanawake na makundi yaliyotengwa au yaliyo katika mazingira magumu huku ukizingatia tamaduni na kanuni za wenyeji.
HALALISHA
Thibitisha na jumuiya ambayo wameianzisha, kupitia taratibu za kimila za kufanya maamuzi, watu binafsi au taasisi zitakazowawakilisha katika mchakato mzima wa FPIC.
MBINU BORA YA WILDLIFE WORKS KATIKA UTEKELEZAJI
FPIC kama Msingi wa Ushirikiano wa Muda Mrefu katika Miradi ya MKUHUMI+ ya Brazili
HAKIKISHA UPATIKANAJI SAWA WA TAARIFA
KANUNI
Fanya kazi na washikadau wa jamii ili kuunda na kusambaza taarifa zinazohitajika kwa maamuzi yao ya kuzingatia taarifa sahihi kuhusu kuanzisha na kuunda mradi wa REDD+.
SAWASISHA UPATIKANAJI WA TAARIFA
Fanikisha na wezesha upatikanaji wa taarifa kwa uwazi, ukamilifu na usawa kwa washikadau wote kuhusu mchakato na matarajio ya REDD+ unaopendekezwa, kwa kuhakikisha kwamba inatolewa au kubuniwa pamoja kwa njia zinazofaa na zinazoombwa kwa makundi yote ya jamii.
Tumia tafiti zisizoegemea upande wowote ili kuthibitisha kuwa jamii inajiamini katika uwezo wake wa kiufundi ili kushiriki kikamilifu katika mchakato wa FPIC.
Shirikiana kuunda mafunzoau warsha za ziada ikiwa ni lazima.
WEKA UELEWA WA PAMOJA
Thibitisha na jamii kwamba uelewa wa tamaduni tofauti upo ili kuwezesha mchakato wa mashauriano ulio wa haki.
Tumia miundo ya utawala iliyowekwa ya jamii ya idhini kushiriki katika mchakato wa FPIC
Simamia kwa umakini mawasiliano ya pande tofauti ili kuanzisha makubaliano ya pamoja kati ya serikali na jamii.
Wezesha FPIC kutokea kwa wima (ngazi ya serikali hadi jamii) na mlalo (ndani na miongoni mwa jamii).
HALALISHA
Wahoji wanajamii kwa kutumia mbinu za kuondoa upendeleo na uwezeshe tafiti za kujitathmini ili kuthibitisha kuwa walijihisi kuwa tayari kushiriki kikamilifu.
MBINU BORA YA WILDLIFE WORKS KATIKA UTEKELEZAJI
Matumizi ya Kucheza katika Kujifunza na Kushiriki katika REDD+
WEZESHA MICHAKATO NA MAKUBALIANO YALIYOUNDWA KWA PAMOJA
KANUNI
Jenga uhirikiano wa haki katika kuandaa mchakato na matokeo.
KUHAMASISHA UWAZI
Weka kumbukumbu, shiriki na hakikisha, shughuli na maamuzi yanapatikana kwa jamii na washikadau.
Saidia mawasiliano ya uwazi kati ya wawakilishi wa jamii na wanajamii wote. Hili linaweza kuwezeshwa kupitia mashirika na vyama vya kijamii vinavyohusika.
RAHISISHA KUFANYA MAAMUZI KWA HAKI NA USAWA
Hifadhi mifumo ya utawala wa kijamii na michakato ya kidemokrasia, huku ukiimarisha miundo ya utawala iliyopo, kulingana na sheria za kitaifa na vigezo vya haki za binadamu.
Shirikiana ili kubuni mchakato wa ushiriki na kufanya maamuzi na Watu wa Asili, jamii za kienyeji na washikadau wengine wa haki, ambao utatekelezwa katika kila hatua, katika kipindi chote cha mradi.
KUJENGA UWEZO NA USHIRIKIANO
Shirikisha mashirika ya usaidizi (kwa mfano, wawezeshaji wa kitamaduni, washauri wa kisheria na kifedha) na uunde kamati ya majadiliano ya jamii inapohitajika. Inapofaa au kwa ombi, maendeleo ya utaalam wa kifedha na mipango ya kubadilishana maarifa.
Imarisha mifumo ya kufanya maamuzi ya ndani au taasisi kupitia uundaji au uimarishaji wa kamati za mitaa, daima hakikisha ushiriki wa maana wa wanawake na makundi yaliyotengwa.
Tumia mchakato wa Nadharia ya Mabadiliko ya jamii kama msingi wa ushirikiano wa haki wa mradi.
HALALISHA
Wahoji wanajamii kwa kutumia mbinu za kuondoa upendeleo na uwezeshe tafiti za kujitathmini ili kuthibitisha kuwa walijihisi kuwa tayari kushiriki kikamilifu.
MBINU BORA YA WILDLIFE WORKS KATIKA UTEKELEZAJI
Jamii Zinaongoza Katika Uhifadhi wa Misitu kwa kutumia Mfumo wa "Nadharia ya Mabadiliko"
MAWASILIANO YA UWAZI, YANAYOJUMUISHA
KANUNI
Kufikia makubaliano kunafuata taratibu wazi za mawasiliano na mazungumzo jumuishi, na ya usawa na uthibitishaji kutoka kwa washikadau mbalimbali.
SAMBAZA
Unda mawasiliano ya wazi, na usambaze kwa upana nyenzo zinazofaa kiutamaduni, kupitia njia mbalimbali zinazoweza kufikiwa na makundi yote, ikiwa ni pamoja na wale waliotengwa.
KUZA HATUA ZA PAMOJA
Heshimu mchakato wa makubaliano kama njia ya kurudia, inayojumuisha kujifunza kutoka kwa shughuli zote za FPIC.
Fuata mchakato wa maafikiano unaoongozwa na jamii kulingana na mahitaji yao, wenye misururu ya kutosha ya maoni, unyumbufu na uwajibikaji.
Ruhusu muda wa kutosha wa majadiliano, maoni na shughuli za maafikiano
KUBALI NA UTIE SAINI
Thibitisha idhini ya jamii kwa ajili ya majadiliano juu ya uidhinishaji wa mradi, utekelezaji, na ugavi wa mapato, unaotokana na matokeo ya tathmini ya athari (SBIA).
Buni kwa pamoja majadiliano na uthibitisho wa makubaliano ya mradi wa REDD+, kwa kutumia lugha za kimataifa na za kienyeji kama ilivyokubaliwa kwa pamoja.
HALALISHA
Thibitisha na jamii:
- Uamuzi huo ulichukuliwa bila kulazimishwa kwa namna yoyote.
- Makubaliano hayo yalijadiliwa kwa mujibu wa mchakato uliokubaliwa.
- Wanaelewa haki zao, ikiwa ni pamoja na haki ya kusema hapana.
- Wanahisi kuwa walikuwa na uwezo wa kutosha wa kitaasisi na kiufundi kujadili makubaliano.
- Walichukulia mchakato wa FPIC kuwa unaofaa kitamaduni na unaojumuisha wanajamii wote.
- Wanajamii wote wanaelewa vipengele vyote vya makubaliano yaliyojadiliwa na athari zake.
- Wanafahamu kikamilifu hatari, majukumu, na wajibu unaoambatana na utekelezaji wa mikataba.
MBINU BORA YA WILDLIFE WORKS KATIKA UTEKELEZAJI
FPIC katika Mradi wa Gerbang Barito REDD+ nchini Indonesia
UFUATILIAJI NA MAONI KWA AJILI YA MABORESHO ENDELEVU
KANUNI
Maoni endelevu na uboreshaji
UNDA USIMAMIZI UNAOJITEGEMEA
Anzisha mchakato unaoongozwa na jamii, unaojitegemea wa kufuatilia utekelezaji wa mradi na kusimamia makubaliano ya ndani ya jamii na upatanishi. Hakikisha kwamba jamii inapatiana idhini endelevu katika kipindi chote ya mradi.
WEKA TARATIBU ZA MALALAMISHI
Kubaliana na jamii kuhusu mrejesho, usuluhishi, na ufuatiliaji wa taratibu zinazofaa kitamaduni kwa ajili ya makubaliano yaliyotekelezwa.
Weka utaratibu unaoweza kufikiwa wa malalamiko kwa ajili ya kuripoti maoni yasiyojulikana.
RAHISISHA MAZUNGUMZO YA WAZI
Weka utaratibu wa kuwezesha mazungumzo yanayoendelea, ya wazi na ya pande mbili kati ya jamii na mwekezaji wa mradi ili kuhakikisha kwamba FPIC inakuwa mchakato unaoendelea.
MBINU BORA YA WILDLIFE WORKS KATIKA UTEKELEZAJI
Kuendesha Meli ya Maendeleo Endelevu: Utawala wa Jamii katika Mradi wa Kasigau Corridor REDD+